Sunday, 7 June 2015

Kwenye Mahafali Tukasa Mwl Nyerere walinyoosha mikono na walisema Amina kwa Wimbo huu wa Kwaya


Hata matching ilikuwepo baada ya kumaliza mahafali ya Tukasa Mwl Nyerere leo

Wanakwaya wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni,wakiongoza matching mara baada ya sherehe za mahafali ya Tukasa, tawi la Chuo cha Mwl Nyerere kumalizika, leo mchana.

Mwisho wa Honeymoon

Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni Mr Mika akimlisha keki mke wake katika mahafali ya Tukasa, Tawi la Mwl Nyerere, leo mchana, Wote ni waimbaji wa kwaya ya kanisa la Kigamboni

Mama na Mwana

Mama na mwana wakilishana Keki katika mahafali ya Tukasa katika Tawi la Chuo cha Mwl Nyerere, leo mchana. Mama na mwana wote ni waimbaji mahiri katika kwaya ya Waadventista Wasabati Kigamboni

Baada ya mazoezi kivulini kwaya imewasilisha ujumbe kwa njia ya wimbo

Sehemu ya wanakwaya wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni wakiwasilisha ujumbe kwa njia ya wimbo katika mahafali ya  Tukasa katika Chuo cha Mwl. Julius Nyerere, leo mchana.

Mazoezi chini ya kifuli kitulivu

Baadhi ya wanakwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni wakijifua chini ya kivuli kabla ya kutoa ujumbe katika Mahafali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mwl Nyerere leo mchana

Monday, 27 April 2015

Habari mpendwa katika Bwana,
Unakumbushwa kwa mara nyingine tena ile siku yenye mibaraka ya pekee imekaribia ni jumamosi ya tarehe 2/5/15 katika kundi la Puna, andaa kipoza njaa,na nauli uanze kutoa mapema siku ya maombi Jumatano kwa Mkurugenzi au Katibu wa Idara ili kupata idadi kamili ya watakaohudhuria siku hiyo.
Barikiwa na uchukue hatua.

Katibu wa Idara ya Vijana-Kigamboni

Thursday, 23 April 2015

tangazo kutoka idara ya vijana

Tarehe 02/05/2015 Jumamosi ndiyo siku ya Vijana kutembelea kundi la Puna,
hivyo kila kijana anapaswa aandae nauli ya kwenda na kurudi ambayo ni 4000/-
pia usisahau kuja na kipooza njaa ni muhimu sana ili kuweza kufurahia baraka za  Bwana
Usipange kukosa ibada hii ya Pekee

Tangazo hili linatoka kwa Uongozi wa Idara ya Vijana-Kigamboni

Thursday, 2 April 2015

Tangazo kutoka Idara ya Vijana

Idara ya Vijana ilitangaza kutakuwa na mafunzo kwa Vijana kutoka wakufunzi mbalimbali.
Mafunzo hayo yatakuwa yakianza  saa 2.00 asubuhi mpaka 9.00 mchana,kumbuka kubeba
kipoza njaa.

Uongozi wa Idara ya Vijana

Tuesday, 31 March 2015

Ujumbe kutoka idara ya Vijana Kigamboni

Habari za Asubuhi
Kutana na Dr. J. Layaa.Sister Ester Muganda na M.G. Mwangi pamoja na wakufunzi wengine wengi katika mafunzo ya vijana kwa Siku ya Jumapili 29/3/15 na 30/03/15,kanisani Kigamboni,
Mada kemkemu zitawasilishwa na kujadiliwa,usipange kukosa ukisoma ujumbe huu hebu mpe habari
njema hii na kijana mwingine. Muda Utajulishwa

Ujumbe huu ni kutoka kwa uongozi wa kanisa Kigamboni

Sehemu ya wanakwaya wa Kanisa la Kigamboni